Msanii mrembo, Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mshindi wa tuzo za MTVMAMA2015, Diamond Platinumz, amejuta kumfahamu msanii huyo baada ya kushinda tuzo hizo.

Kidoti ameonesha kuumizwa na post ya Diamond yenye kijembe kwa wahasimu wake ikiwa na video inayomuonesha mrembo huyo akiimba na kucheza wimbo wake ‘Mdogomdogo’ tena kwenye kibwagizo chenye dongo kwa watu wanaomuonea wivu. Post iliyosindikizwa na maandishi, “Mbona Bado Mtanyooka tu…”

Jokate ambaye hivi sasa anaonekana kuwa na uhusiano wa karibu sana na Ali Kiba ambaye imeonekana wazi kuwa ni hasimu mkubwa wa Diamond licha ya wao kukanusha, aliamua kujibu huku akielelza kuwa mwimbaji huyo ana tabia ya kuwadhalilisha wanawake bila sababu za msini.

Hiki ndicho alichoandika Jokate Kidoti kwenye Instagram:

Tuki-support mtu ndio kama hivi matokeo yake mtu anatumia baadae kukudhalilisha. Hii video aliyo-post kwanza ni #TBT kama sijakosea mwaka jana mwishoni nilikuwa sehemu na my friends @bikira_wa_kisukuma akani-record na kumtumia @diamondplatnumz bila mimi kujua. Kiukweli sijui kwanini walifanya hivyo. Nikaja kujua baadae sana na nikaona sio big deal cause kila mtu anapenda mziki na sio dhambi kucheza mziki wowote uupendao.

Ila kitendo cha @diamondplatnumz kwenda kuitafuta huko ilikokuwa hii video clip na kui-post leo najiuliza maswali mengi 1, anataka ionekana kama nilikuwa nashangilia ushindi wake? Which is not bad hakuna ubaya hapo kama unaamini ushindi wake ni sifa kwa taifa ila 2, Kwanini a-post na caption ya Na Bado Mtanyooka? Ili amkomoe nani?

Au kwasababu niko karibu saaana na @alikibaofficial anatafuta kutuchonganisha? Ili iweje? Mimi I believe life goes on na kila mtu ana uhuru wa kumpenda au kuwa karibu na yule apendaye na kum-support ndio maana hata mimi nimekuacha na your new life 3, Pengine ni kweli anaendeleza zile hulka zake za kudhalilisha wanaweke aliokuwa nao waonekane sio kitu just because hawako na diamond platnumz chibu dangote.

Which to me is just dead wrong. @diamondplatnumz hizi sio tabia tunazozitegemea kwa mtu anayejisema anakomboa mziki wa Tanzania sio kwa kuweka visasi na fitna zako wazi wazi hivi. Unatu fanya tukose imani nawewe zaidi na tunaogopa ku-support cause hukawi kutugeuka. Kuwa tofauti basi, onyesha mfano kwamba kweli hupendi beef unapenda mziki wa Tanzania uendelee ila kwa ulichoki-post unaonyesha wazi UNA visirani na hutaki mema unatafuta drama, kiki, vurugu unataka kila siku uwe wewe tu ambazo kiukweli mimi binafsi siziwezi utaendelea kushinda wewe tu katika hilo na sitashindana nawewe katika hilo kwasababu siwezi nawewe unajua kama ulivyoniimba mimi mpole, sinaga maneno ( ila kwenye kazi ndio nakuwa mkali kama pilipili ). Ila ungetumia busara kidogo. Just move ON kiroho safi.

Naomba pia nitumie fursa hii kukupongeza kwa tuzo yako ya MTV ila @babutale hata wewe ndugu yangu? Is this how tunaendeleza so called uzalendo? Inshallah Kheri lakini yote maisha wanyonge sisi iko siku Mungu atatunyanyua.?

Miley Cyrus Atangaza Kusherehesha Tuzo Za Video Za MTV ‘MTVMA’
Mastaa Wawili Watangaza Kupata Watoto Kwenye Tuzo Za MTV/MAMA2015