Tuzo za MTVMAMA 2015 zilizofanyika July 18 mwaka huu, Durban, Afrika Kusini ziliambata na matukio muhimu ya furaha kwa mastaa waliopanda jukwaani kuchukua tuzo walizoshinda.

Mkali wa ‘Aye’, Davido aliweka wazi kuwa amepata mtoto hivi karibuni. Alitoa tangazo hilo alipokuwa akitoa speech ya kupokea tuzo ya ‘Mwimbaji Bora wa Kiume Afrika’. “I wanna tell my new born baby, daddy is bringing the toy at home,” alisikika Davido baada ya kuwashukuru mashabiki na kuwatia moyo wasanii wenzake aliokuwa akishindana nao kwenye kipengele hicho ambao ni Davido, Wizkid na AKA.

Naye rapper wa Afrika Kusini, AKA aliyeshinda tuzo ya wimbo bora wa kushirikishana kupitia wimbo wake ‘All Eyez On Me’ aliomshirikisha Burna Boy, aliiambia dunia kuwa ana mtoto wa kike aliyempata hivi karibuni na ana-dedicate tuzo hiyo kwake.
MTV-MAMA14

Diamond na Vanessa Mdee waliiwakilisha Tanzania kwenye tuzo hizo kubwa Afrika. Diamond alifanikiwa kushinda tuzo ya mtumbuizaji bora wa mwaka (Best Live Act) ikiwa ni moja kati ya vipengele vitatu alivyotajwa.

Jokate Ajuta Kumfahamu Diamond
Ester Bulaya Aimwaga CCM