Aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans, Dokta Jonas Tiboroha amelamba dili katika klabu ya Stand United ya mkoani Shinyanga.

Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu ya Stand United, Muhibu Kanu alisema wameridhishwa na uzoefu na uwezo wa Toboroha pamoja na taaluma yake kwa ujumla.

Alisema tayari Tiboroha amekubali kufanya nao kazi hasa baada ya kuafikiana katika masuala mbalimbali ya ajira hiyo.

“Stand sasa inakwenda kuwa kampuni kwa hiyo ili kuendana na hadhi hiyo tumelazimika kuimarisha sekretarieti kwa kuajiri wataalamu watakaotusaidia,” alisema Kanu.

Hata hivyo Dokta Tiboroha ameibua maswali kwa wana Yanga hasa kufuatia kauli aliyoitoa hivi karibuni wakati akiachana na Yanga ya kwamba anakabiliwa na kazi za Serikali katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, hivyo hatoweza tena kujihusisha na masuala ya soka kwa sababu yanampunguzia umakini wa ajira yake ya uhadhiri.

Tiboroha alijiuzulu nafasi yake ya ukatibu ndani ya Yanga kwa madai ya kutokuwa na maeleano mazuri na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Yusufu Manji, ingawa mwenyewe hakuweka wazi.

Wabunge waugomea utaratibu wa ofisi ya Bunge, wadai sio wanafunzi
Toto Africans Washikishana Adabu Jijini Mwanza