Kiungo kutoka nchini England, Jonjo Shelvey amesema hatoisaliti klabu ya Newcastle United, ambayo ilimsajili mwanzoni mwa mwaka huu, akitokea Swansea City kwa ada ya uhamisho wa Pauni million 12.

Jonjo ameweka bayana suala hilo, katika kipindi hiki kigumu ambacho wachezaji wa Newcastle Utd wanaendelea kuhangaikia namna ya kuinusru klabu yao isishuke daraja.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 amesema hata kama itatokea klabu hiyo inashindwa kujinusuru katika janga la kushuka daraja, hatokua tayari kuisaliti kutokana na kuamini aliaminiwa na ndio maana akasajiliwa klabuni hapo.

Amesema ni vigumu kwa wachezaji wengi kuweka msimamo kama huo, hususana katika kipindi hiki cha kuelekea ukingoni mwa msimu, lakini kwake anaamini hakuna litakalo shindikana, hata akicheza ligi daraja la kwanza msimu ujao, kwani anaamini atakua sehemu ya watu watakaoirejesha The Magpies ligi kuu kwa mara nyingine.

Mbali na kuweka msimamo huo, pia amewatahadharisha viongozi wa klabu nyingine za ligi kuu, kutojisumbua kumfuata itakapotokea Newcastle Utd inashuka daraja, kwani hatokua tayari kuondoka St James’ Park.

Newcastle Utd bado wana nafasi ya kujinasua kwenye mtihani wa kushuka daraja msimu huu, kutokana na idadi ya michezo sita iliyosali ambapo watatakiwa kushinda yote ili kujikusanyia point 18.

Katika msimamo wa ligi Newcastle Utd ambayo inanolewa na meneja kutoka nchini Hispania Rafael Benitez, inashika nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi kwa kufikisha point 25.

Anne Kilango auelezea Moyo wake baada ya kung'olewa Ukuu wa Mkoa
Washambulia Mahakama kwa Risasi Geita kukwamisha ushahidi wakati kesi ikiendelea