Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli ametangaza vita dhidi ya viongozi wa chama hicho wanaojinufaisha na mali za chama.

Akizungumza jana na na watumishi wa chama hicho katika ukumbi wa makao makuu ya chama maarufu kama ‘White House’, Dkt. Magufuli aliwataka viongozi waliokuwa wakitumia vibaya madaraka yao kujinufaisha na mali za chama kuanza ‘kuzitema’.

Alisema kuwa chama hicho tawala kina rasilimali nyingi na vyanzo vya mapato vinavyoweza kukifanya kuwa na fedha nyingi za kujiendesha ikiwa ni pamoja na kuboresha malipo ya wafanyakazi lakini wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakijichumia mali hizo kwa maslahi binafsi.

Mwenyekiti huyo wa CCM alisema kuwa ni bahati mbaya kwa viongozi wa aina hiyo kuona kuwa amechaguliwa kushika wadhifa huo kwani muda wao umekwisha. Alisisitiza kuwa anazungumza hayo kwa sababu anayafahamu.

“CCM ni chama kikubwa chenye mali na rasilimali nyingi, lakini ninashangaza kuona wanachama wake au chama chenyewe kinakuwa ombaomba, katika uongozi wangu siwezi kukubaliana na jambo hilo hata kidogo,” alisema.

Aidha, Dkt. Magufuli aliahidi kuboresha kipato cha watumishi wa chama hicho hususan wa kima cha chini akieleza kuwa changamoto ya kipato wakati mwingine huwa chanzo cha watumishi hao kushawishika kirahisi kukihama chama hicho.

Dkt. Magufuli alikabidhiwa rasmi Uenyekiti wa chama hicho Julai 23 mwaka huu baada ya Dkt. Jakaya Kikwete kung’atuka rasmi.

->>>Waziri Mkuu: Uamuzi wa kuhamia Dodoma siyo siasa

Nay wa Mitego aanza ‘kufunguka’ baada ya BASATA kumfungia kufanya muziki
Video: Meya Wa Manispaa Ya Kinondoni Atumbua Majipu