Kocha Juma Mwambusi ameandika barua ya kujiuzuru kuifundisha timu Mbeya City, kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo kwenye michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu.

Kikao cha Bodi ya Mbeya City FC kilichofanyika leo Jumamosi kwa pamoja kimeridhia ombi la kocha huyo kujiuzuru.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba Mwambusi aliwasilisha ombi la kujiuzuru tangu Novemba 26 mwaka huu kwa maslahi mapana ya klabu kufutuatia mwenendo usioridhisha wa timu tangu kuanza.

“Katika kipindi hiki cha mpito Bodi yetu imemkabidhi timu Kocha Msaidizi Mohamed Kijuso huku mchakato wa kumtafuta kocha mkuu ukiendelea” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, James Kasusura.

Taarifa hiyo ilieleza zaidi kwamba Bodi inamshukuru Mwambusi kwa mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya timu na bado inahitjai ushauri na uzoefu wake katika tasnia ya michezo.

Mbeya City inashika nafasi ya 18 ikiwa na pointi nane katika michezo 12 waliyocheza.

Man City wavutwa shati England
Simba SC yamtimua Aussems , yataja sababu mbili

Comments

comments