Mbunge wa Kauinti ya Kapseret nchini Kenya, Oscar Sudi ameziomba mamlaka za usalama kutomfungulia mashtaka Kijana David Chege (17), ambaye aliiba ndege ya jirani yake iliyokuwa imepaki na kisha kuirusha hewani akiahidi kumpeleka shule ya urubani.

Mbunge Sudi ametoa ombi hilo, baada ya kijana Chege kudaiwa kuingia kwa siri kwenye nyumba ya jirani yake huyo mzungu na kuingia eneo la rubani na kuiwasha kisha kuirusha kwa dakika kadhaa kabla ya kuparamia miti na kutua.

Kijana David Chege, aliyeiba Ndege ya jirani yake, kulia ni Ndege hiyo aina ya PA25 yenye namba 5Y-AZA. Picha ya Mwakilishi.com

Amesema, “naomba Serikali imsamehe huyu kijana kutoka Gilgil asishtakiwe, tafadhali mnipatie ili nimpeleke katika chuo cha kujifunza mambo ya kuwa rubani, nnahidi kuhakikisha kuwa nitamsimamia kusoma urubani.”

Ijumaa Machi 24, 2023 katika eneo la Balolow lililopo Ndume Gilgil, Kijana Chege anadaiwa kuingia kwa siri kwenye nyumba ya mzungu na kufaulu kuiwasha ndege hiyo aina ya PA25 yenye namba 5Y-AZA kisha kuirusha angani.

Jean Baleke apewa dozi maalum Simba SC
Kocha Ihefu FC aitahadharisha Simba SC