Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kuahirisha maandamano yaliyokuwa yakiendelea kufanywa na muungano wa vyama vya upinzani, NASA dhidi ya tume ya uchaguzi nchini humo IEBC huku kukiwa na madai ya maafisa wa polisi kutumia nguvu zaidi dhidi ya waandamanaji.

Odinga amesema kuwa uamuzi huo ni kufuatia vifo vya baadhi ya wafuasi wake ambao alidai walipigwa risasi na polisi. Amesema muungano huo utatoa mwelekeo wake baada ya siku ya Mashujaa itakayofanyika Ijumaa .

Odinga amemlaumu Waziri wa Usalama nchini humo, Fred Matiangi na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Joseph Boinet akiwashutumu kwa kuwaagiza maafisa wa polisi kuuwa raia wasio na hatia.

”Siku ya Ijumaa tutawakumbuka raia wasio na hatia kama mashujaa kwa harakati dhidi ya haki ya uchaguzi katika eneo ambalo tutalitaja baadaye. Siku hiyo tutatangaza hatua tutakayochukua”, amesema Odinga.

Amesema kuwa wanawataka maafisa wa polisi kukomesha mauaji hayo ambayo amesema kuwa ni gharama kubwa kwa taifa.

”Serikali lazima isitishe ushirikiano wa maafisa wa polisi na majambazi mbali na ukiukaji wa kikatiba wa kuwapeleka polisi kuwakabili wafuasi wa NASA”, amesema.

Aidha, Mahakama kuu ilisitisha kwa muda marufuku ya Serikali dhidi ya maandamano ya IEBC katikati mwa miji ya Nairibi, Mombasa na Kisumu.


Video: NGWEA, NURAH walikuwa mbele ya muda – Zaiid, afunguka siri ya ‘WOWOWO’

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 18, 2017
Nicki Minaj aeleza alichowaandalia mashabiki wake