Meneja wa muda wa klabu ya Aston Villa, Kevin MacDonald amerejesha maneno ya vijembe yanayoendelea kutolewa na baadhi ya watu ambao hawakupendezwa na hatua iliyochukuliwa na viongozi wa klabu hiyo dhidi yake.

MacDonald mwenye umri wa miaka 54, anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Aston Villa kama mkuu wa benchi la ufundi mwanzoni mwa juma lijalo, ambapo The Villians watakua wageni wa Tottenham Hotspur.

MacDonald, amesema jambo la kuaminiwa na wengi sio suala la kupewa nafasi kwake kwa sasa, bali anachotazama ni kuhakikisha mambo yanakaa sawa katika mchezo ujao.

Amesema kukubaliwa na wengi hakumaanishi kama ushindi unaweza kupatikana kirahisi, bali inapaswa kila mmoja kuonyesha ushirikiano ili mafanikio yaonekane klabuni hapo.

Mzozo baina ya wanaompinga MacDonald, umeibuka kufuatia viongozi wa Aston Villa kushindwa kumpata mbadala wa Tim Sherwood ambaye alitimuliwa mwishoni mwa juma lililopita, kutokana na kushindwa kufikia lengo la kusaka ushindi kama ilivyotarajiwa tangu alipotangazwa kuwa meneja huko Villa Park February 14 mwaka 2015.

Bomu Lilitegwa Kituo Cha Polisi Lazua Taharuki Zanzibar
Scholes Ampa Makavu Live Louis Van Gaal