Kocha Kinnah Phiri aliyekuwa akikinoa kikosi cha Free State ya Afrika Kusini ametua Mbeya City na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Katibu Mkuu wa City, Emmanuel Kimbe amethibitisha taarifa hiyo na kwamba Phiri alitua jijini Mbeya jana jioni na leo jioni anatarajia kuanza kazi huku Meja Mstaafu Abdul Mingange akipumzishwa.

Kimbe ameiambia BOIPLUS kuwa “Phiri atasaidiana na watu wengine waliopo kwenye benchi la ufundi kwani Mingange hatutakuwa naye tumeona apumzike kutokana na matatizo ya kifamilia yaliyokuwa yakimkabili,”.

Kimbe alisema kuwa moja ya kazi ambazo Phiri anatakiwa kuzifanya ni kuhakikisha anaibakisha timu kwenye ligi kwani matokeo wanayoyapata si mazuri kwao jambo analoamini kwamba litawezekana kutokana na uwezo mkubwa alionao kocha huyo.

Phiri aliyezaliwa miaka 61 iliyopita jijini Blantyre Malawi ndiye aliyemsajili Mrisho Ngassa katika klabu ya Free State.

Waamuzi Waanza Kunyooshewa Vidole Ligi Kuu
Askofu ashusha Ombi kwa Magufuli, ataka hawa waliotumbuliwa wasamehewe