Shirikisho la mchezo wa riadha nchini Tanzania RT limethibitisha kukamilika kwa maandalizi ya michuano ya mbio za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Mjini Moshi February 28 mwaka huu.

Kaimu katibu mkuu wa RT Ombeni Zavalla amesema mapaka kufikia leo maaandalizi yote yamekamilika na njia zitakazo tumika katika mbio hizo zimeshaandaliwa huku tayari washiriki mbalimbali kutoka nje ya Tanzania wakiwa wameshaanza kujiandikisha tayari kushiriki michuano hiyo.

Zavalla amesema kwa sasa kilichobaki ni washiriki tuu kupimwa afya zao kwa ajili ya kuzuia wale wenye kutumia dawa za kusisimua misuli katika mbio hizo.

Jerry Muro Amjibu Hadji Sunday Manara
Spurs Wapewa Ruhusa Ya Kujenga Uwanja Jijini London