Mratibu wa shughuli za kampeni wa chama cha ACT- Wazalendo wilayani Misungwi mkoani Mwanza, John Mbozu ameswekwa rumande kwa kosa la kupiga picha kituo cha kupigia kura cha Kata ya Kijima.

Mbozu ambaye pia ni Katibu wa Mambo ya Nje wa ACT-Wazalendo amepelekwa kituo cha polisi cha Misasi kwa mahojiano zaidi.

Aidha, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Eliud Mwaiteleke amesema kuwa hakuna tukio lolote lililoripotiwa kukwamisha upigaji kura huku mtu mmoja akikamatwa kwa kosa la kupiga picha kituo hicho bila kibali.

Hata hivyo, wakazi wa Kata ya Misasi wanapiga kura leo kumchagua diwani kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Kwabi Panduji (CCM)

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 27, 2017
JPM amuandikia barua Rais wa China