KMC FC imeshindwa kufurukuta ugenini dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Black Rhino mjini Karatu mkoani Arusha leo Jumatano (Septemba 29).

Polisi Tanzania waliokua wanautumikia Uwanja wa Black Rhino kama nyumbani, wameanza vyema Msimu wa Ligi Kuu kwa kuichapa KMC FC mabao 2-0.

Mabao ya Maafande wa Polisi yalipachikwa wavuni na Mshambuliaji wao mpya Vitalis Mayanga katika dakika ya 3 na 20.

Mayanga amejiunga na Maafande wa Polisi ambao maskani yao ni mkoani Kilimanjaro, akitokea Kagera Sugar ya mkoani Kagera baada ya mkataba wake kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita 2020/21.

Polisi Tanzania watacheza mchezo wa mzunguuko wa pili mwishoni mwa juma hili dhidi ya Azam FC, huku KMC FC wakitarajia kucheza dhidi ya Coastal Union ugenini jijini Tanga.

Moto wazuka Shule ya Nyehunge
Muhagama asisisitiza mifumo ya usalama na afya kuboreshwa