Kocha Mkuu wa Man Utd Erick ten Hag amelaani makosa ya kiakili ambayo yalichangia kufungwa kwa kikois chake dhidi ya Galatasaray ya Uturuki katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya uliochezwa juzi Jumanne (Oktoba 03).

Mashetani Wekundu walikuwa mbele mara mbili wakati wa nchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, lakini hatimaye walipoteza 3-2 baada ya makosa kadhaa ya safu ya ulinzi ikiwa moja la Andre Onana na kumfanya Casemiro kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu eneo la hatari.

Kipigo hicho kilikuwa cha sita kwa United katika msimu huu ambao umekuwa mbaya zaidi hadi sasa, na klabu hiyo iko mkiani katika kundi lake baada ya kufungwa mechi zao mbili walizocheza.

Akizungumzia kufungwa huko kupitia TNT Sports, Ten Hag alisema kulikuwa na makosa ambayo wachezaji wake walifanya usiku huo.

“Tulifanya makosa ya kiakili, huwezi kuyaruhusu katika kiwango hiki. Unaadhibiwa. Hii ni ngumu kudhibiti. Sote tuko pamoja katika hili. Tulikuwa juu mara mbili na kudhibiti mchezo. Tunatarajia zaidi pamoja.”

Kosa moja kama hilo lilitoka kwa nyota Marcus Rashford. Huku timu yake ikiwa sare ya 1-1 katika kipindi cha pili, mshambuliaji huyo alibaki yeye na beki, lakini badala ya kupiga shuti, akajaribu kutoa pasi kwa Bruno Fernandes, pasi ambayo haikuwa na matokeo chanya.

Ten Hag alitoa maoni yake juu ya tukio hilo, akisema: “Hiyo ni juu ya Marcus. Kwa wakati kama huo lazima afanye uamuzi.”

Nishati: Serikali kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji
Ziara ya Rais India: Tanzania kuanzisha Kiwanda cha Simu janja