Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes leo inashuka uwanjani kucheza mtanange wa nusu fainali dhidi ya michuano ya CECAFA dhidi ya Sudan mchezo ambao utapigwa katika jiji la Kampala.

Kocha wa timu hiyo ya vijana Zuberi Katwila amesema mipango yao ni kuweza kuibuka na ubingwa wa michuano hivyo basi ni muhimu kupata ushindi dhidi ya Sudan.

Katwila amesema atatumia muda wa dakika 10 ili kuwachunguza wapinzani wao na kujua mbinu ambazo kiufundi zitampa nafasi nzuri ya kubaini ubora na udhaifu wa timu ya Sudan.

”Itakua mechi ngumu kila timu iliyofika nusu fainali ni bora. Tuliwaona Sudan kidogo pia tumepata taarifa zao, ninajua tutatumia mbinu gani kupata ushindi,” alisema Katwila.

Nusu fainali nyingine ni Kenya ambapo itachuana na Eritrea katika uwanja wa kituo cha ufundi Njeru ambapo Kenya ilifunga Burundi mabao 2-1hadi kufikia hatua hiyo wakati Eritrea wakiichapa Zaznibar 5-0.

Video: DC Mjema aagiza polisi 'kuwagonga Dada Poa', Radi yaua wanne wakinywa pombe
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 2, 2019