Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba SC, Mwalami Sultan ‘Shilton’ ametajwa kwenye orodha ya watuhumiwa tisa wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi kwa kukamatwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye jumla ya Kilo 34.89.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) Gerald Kusaya ametangaza orodha ya watuhumiwa hao katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Jumanne (Novemba 15) jijini Dar es salaam.

Kusaya amesema watuhumiwa 9 wanaongozwa na Mmiliki wa Kituo cha kulea na kuendeleza vijapi vya soka kwa vijana cha Kambiaso Sports Academy, Alhaj Kambi Zubeir Seif.

Amesema watuhumiwa hao wote Tisa wamekamatwa katika maeneo mbalimbali hapa hapa ndani ya nchi katika Operesheni iliyofanyika mwezi Oktoba mwanzoni na November 2022.

Kabla ya kurejea Simba SC kama Kocha wa Makipa Mwalami Sultan ‘Shilton’ alikua muajiriwa na Kituo cha kulea na kuendeleza vijapi vya soka kwa vijana cha Kambiaso Sports Academy chini ya Kocha Mkuu Mecky Mexime aliyetimkia Kagera Sugar mwanzoni mwa mwezi huu.

Wengine waliotajwa katika kesi hiyo ni Said Abeid Matwiko (41), Maulid Mohamed Mzungu (54), John Andrew Chipanda (40), Rajabu Mohamed Dhahabu (32), Seleman Matola Said (24), Hussein Mohamed Pazi (41) na Ramadhan Rashid Chalamila (27).

Wauhumiwa wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili.

Wataalamu wa Mifugo kujengewa uwezo huduma Vijijini
Tisa wanaswa na dawa za kulevya Dar