Aliyekuwa kocha wa klabu ya Everton, Ronald Koeman amesema kuwa kushindwa kumsaini mshambuliaji Olivier Giroud kutoka Arsenal msimu huu ni moja kati ya sababu zilizochangia kutimuliwa kwake katika klabu hiyo.
Koeman amesema Giroud mwenye umri wa maiaka 31 alikaribia kutua Goodison Park na angekuwa mbadala sahihi wa Romelu Lukaku lakini dakika za mwisho kabla ya makubaliano kukamilika Giroud aliamua kubaki Arsenal.
”Lukaku alikuwa muhimu kwetu hasa kwa mtindo wake wa uchezaji, Giroud angetufaa sana kwani anacheza sana mipira ya juu tofauti na Rooney na Nicola Vlasic ambao wanasubiri mpira uwafate miguuni tu,” alisema Ronald Koeman.
-
Claude Puel ataeuliwa kuwa kocha mpya Leicester City
-
Florentino Perez amgwaya Harry Kane
-
Ronald Koeman atoa neno la shukurani, aiombea kheri Everton
Everton ilitumia kiasi cha Pauni milioni 150 katika usajili kwa kuwanunua kiungo Gylfi Sigurdsson kwa £45m, goalkeeper Jordan Pickford kwa £30m, mlinzi Michael Keane kwa £30m na kiungo Davy Klaassen kwa £24m.
Pamoja na usajili huo Eveton chini ya Ronald Koeman ilishindwa kupata mtokeo mazuri jambo lililopelekea kocha huyo kutimuliwa akiiacha Everton katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Epl.
Kocha David Unsworth tayari amechukua nafasi ya Koemana kama kocha muda wa klabu hiyo na katika mchezo wake wa kwanza alipata kipigo cha mabao 2-1 akicheza katika uwanaja wa Goodison Park dhidi ya Chelsea kwanye michuano ya Carabao Cup.