Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ameielekeza Halmashauri ya Kondoa mkoani Dodoma kumaliza miradi ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi ifikapo Julai 15, 2023.

Jafo, ametoa maelekezo hayo hii leo Mei 9, 2023 alipofanya ziara ya kukagua shughuli za Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza usalama wa chakula (LDFS) na kubaini kutokamilika kwa uchimbaji wa visima virefu vya maji safi wakati tayari Serikali ilishapeleka fedha.

Amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu miradi na kutoa fedha ili wataalamu wa halmashauri watekeleze miradi lakini wameonesha kusuasua na hivyo wananchi kukosa huduma ya majina kwamba suala mazingira ni mtambuka hivyo lengo la mradi ni kuwanufaisha wananchi ili waweze kufanya shughuli mbadala za kiuchumi na kuachana na shughuli zinaazohusiana na uharibifu wa mazingira.

“Mkurugenzi nakutegemea kusimamia wataalamu wako wa halmashauri na RUWASA Kondoa ili uchimbaji wa visima ukamilike kwa wakati wananchi wamechoka kusubiri toka mwezi Oktoba mpaka leo mnasuasua wakati Serikali tayari ilishawaletea fedha,“ alisema.

Aidha ameongeza kuwa, Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu miradi inayohusisha ufugaji, kilimo, maji na ardhi ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hivyo lazima kulinda mazingira na ndiyo maana Serikali ikapeleka mradi huu kwa wananchi wa halmashauri hiyo ili
wapate shughuli mbadala za kiuchumi za kufanya pamoja na kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

Watatu wafa maji Geita, DC awapa angalizo wavuvi
Polisi wa Tanzania kupata mafunzo nchini Korea