Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Lionel Messi amefuta fikra za mashabiki wengi duniani ambao wanaamini kikosi cha FC Barcelona hupata wakati mgumu pale wanapokua nje ya kikosi cha mabingwa hao wa Hispania.

Kwa muda mrefu mashabiki wengi wa soka dunia wamekua wakiamini FC Barcelona hupata shida kubwa ya kufikia lengo la ushindi, wanapomkosa Messi.

Mshambuliaji huyo amesema fikra hizo ni potofu na katu hazipaswi kupewa nafasi katika mazungumzo ya shabiki yoyote anaependa soka duniani.

Amesema yeye ni mchezaji kama ilivyo kwa wachezaji wengine klabuni hapo, na amekua akishangazwa na taarifa hizo ambazo amedai huenda zinatengenezwa makusudi ili kuvunja umoja na mshikamano uliopo baina ya wachezaji wa FC Barcelona.

“Kila mmoja FC Barcelona ana uwezo mkubwa na ndio maana yupo hapa, tunapambana kwa pamoja na hakuna anaetegemewa hadi kufikia hatua ya kutokuwepo kwake uwanjani kunaweza kuharibu mipango ya ushindi, hilo sio kweli,”

“Mara kadhaa nimesikia uvumi huo na niliamua kukaa kimya kwa kuamini huenda kuna wakati ungekwisha na mambo mengine kuchukua nafasi yake, lakini linaendelea kuzungumza, hivyo sina budi kulikanusha kwa kusema sio kweli.” Alisema Messi.

Jurgen Klopp Amkaribisha Steven Gerrard
Viwango Vya soka Duniani, Brazil Yaipumulia Argentina