Mwanasiasa na mwanasheria wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ametilia mkazo nia yake ya kugombea urais 2020, endapo atapata wito kutoka kwa wananchi na chama chake kugombea nafasi hiyo.

Lissu ametoa msisitizo huo alipozungumza na chombo cha habari cha VoA, alipokuwa nchini Marekani na kueleza kipaombele chake endapo atapata nafasi hiyo.

” Nimeshatangaza utayari wangu wa kugombea nafasi hiyo nikiteuliwa na chama changu na ninarudia tena nikipata wito wa kugombea urais nitapokea wito huo.” amesema Lissu

Lissu ambaye yupo nje ya nchi tangu mwezi Septemba 7, mwaka juzi kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi ameshikilia msimamo wake huo wa kugombea urais licha ya hivi karibuni kubainisha kuwa hatarejea nchini hadi hapo chama chake kitakapo mhakikishia usalama wake.

Ametaja malengo yake iwapo atafanikiwa kuteuliwa na chama chake kugombea urais, amesema atarejea upya mchakato wa kutengeneza katiba mpya ya wananchi ili kuwapatia wananchi katiba bora.

Lissu amekuwa Mbunge kwa vipindi viwili, alivuliwa ubunge wake mwaka huu kutokana na sabau ambazo spika wa bunge, Job Ndugai alizitoa za utoro bungeni na pia kutokujaza fomu za maadili ya watumishi wa umma ambazo hutakiwa kujazwa pia na wabunge wote.

 

 

 

 

 

Kenya: Mwili wa Padri aliyepotea siku saba wapatikana umefukiwa
Mwakinyo ampiga vijembe bondia wa Manny Pacquaio , 'Samatta, Diamond ni watoto'