Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema anaengwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa amesema kuwa hatakubaliana na matokeo ya uchaguzi wa rais yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC).

Akiongea na waandishi wa habari, Lowassa ameeleza kuwa matokeo hayo yamegubikwa na udanganyifu na wanaoushahidi wa kutosha kuhusu udanganyifu huo. Ameeleza kuwa idadi ya kura za urais za chama hicho zimepunguzwa tofauti na kura zilizopatikana katika vituo vingi. Pia, amesema idadi ya kura za urais zinazotangazwa na NEC haimbatani na matokeo halisi kwenye vituo husika.

Kadhalika, Lowassa ameeleza kuwa kukamatwa kwa timu ya vijana wa Chadema waliojitolea kufanaya majumuisho ya kura kwa njia ya kielekroni (Tallying) kumefanyika makusudi kwa lengo la kuwahujumu matokeo.

Mkwasa Ajitetea Kwa Ibrahim Hajib
Matokeo ya Urais Zanzibar Yafutwa Rasmi