Baada ya kusubiri kwa muda mrefu matokeo ya urais visiwani Zanzibar, Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza kufuta matokeo ya hayo kwa madai kuwa yalighubikwa na dorasi nyingi.

Mwenyekiti wa ZEC, Salim Jecha Salim amesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria ya uchaguzi.

Mwenyekiti huyo wa ZEC ameleza kuwa makamishna wa tume ya uchaguzi wamekuwa wakitofautiana na hata kufikia hatua ya kupigana kutokana na upendeleo fulani. Amesema katika vituo vingine vya kupigia kura kama vile Pemba kura zilizopigwa zilikuwa nyingi zaidi ya kura zilizosajiliwa.

ZEC

Kwa mujibu wa BBC imeamliwa kuwa uchaguzi huo umepangwa kurudiwa baada ya siku 90. Awali, CCM iliwalalamikia CUF kwa madai kuwa wamefanya hujuma katika uchaguzi huo.

Hali ya wasiwasi ilitanda baada ya Tume kuchukua muda mrefu kutangaza matokeo hayo ambayo yanahusisha wapiga kura nusu milioni, ambayo yamefikia siku ya tatu hadi leo huku ahadi ya kutangazwa matokeo hayo kwa muda ikiwa imeshindwa kufikiwa.

Lowassa Apinga Rasmi Matokeo ya Urais
Kinachoendelea ‘Kigoma Kusini’ kwa Kafulila