Mwanasiasa Mkongwe na kada wa Chama Cha Mapinduzi, Pancras Ndejembi amemshauri Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kumuunga mkono Dkt. John Pombe Magufuli aliyechaguliwa na chama hicho kugombea kiti cha urais wa Tanzania.

Akiongea jijini Dar es Salaam jana, Dejembi alisema kuwa yeye ni mmoja kati ya wanachama wa chama hicho waliokuwa wanamuunga mkono Edward Lowassa na kwamba bado anaamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kuiongoza nchi. Lakini kwa kuwa ameona chama chake kimempitisha mtu mwingine, tayari ameshasahau kama alikuwa ‘Team Lowassa’ na hivi sasa anamuunga mkono mgombea aliyepitishwa ambaye ni Dkt. Magufuli.

“Hakuna asiyejua kuwa mimi nilikuwa namsapoti Lowassa. Nilikuwa natumia haki yangu. Lakini siwezi kuiacha CCM eti kwa sababu mgombea niliyekuwa namuunga mkono hakuchaguliwa. Nitabaki CCM na Magufuli ndiye mgombea wetu,” alisema Ndejembi.

Kwa mujibu wa The Citizen, kada huyo wa CCM alimshauri Lowassa kuendelea kukiunga mkono chama hicho na kuacha kujitenga ili kuitunza heshima na uaminifu wake katika chama.

Ushauri wa Ndejebi unakuja huku kukiwa na taharuki kuhusu uamuzi atakaochukua Edward Lowassa baada ya kushindwa kupita kwenye chujio la Kamati ya Usalama na Maadili ya chama hicho.

Jana, kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mweru alitupia lawama Kamati ya Ulinzi na Usalama akidai ilikosa maadili kwa kukiuka katiba ya chama ili wamwage Lowassa na kumchagua mtu wanaemtaka wao kwa maslahi binafsi.

Diamond na Vanessa watajwa tuzo za ‘Entertainment Africa’ za Marekani
Chuba Akpom Amkuna Arsene Wenger