Wakati wanasubiri matokeo ya tuzo za MTV/MAMA2015 zitakazotolewa wiki hii, Durban, Afrika Kusini, Diamond Platinumz na Vanessa Mdee wametajwa tena kuwania tuzo za Entertainment Africa za Marekani.

Wasanii hao wanapigana vikumbo kwenye tuzo hizo na wasanii wakubwa wa Afrika Magharibi.

Diamond Platinumz anawania vipengele viwili ambavyo ni Hottest Male Single of the Year (Ntampata Wapi) akishindana na Davido (Aye), Fally Ipupa (Original), Dellon Francis (Get Low) na R2Bees (Lobi).

‘Best Male Artist of the Year’ ni tuzo nyingine anayowania Diamond, katika kipengele hicho anashindana na Fally Ipupa, Eddy Kenzo, Wizkid na Sarkodie.
Vee

Kwa upande wa Vanessa ‘VeeMoney’ Mdee anawania tuzo ya Best Female Artist of The Year akishindana na Victoria Kimani, Bucie na Yemi Alade.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa October 31, mwaka huu.

Jeremain Lens Kufanya Tena Kazi Na Advocaat
Lowassa Ashauriwa Kumuunga Mkono Magufuli