Takribani watu 22 wakiwemo Wabunge, wamekamatwa kwa kushiriki maandamano yaliyoratibiwa na Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga ambayo yaliharamishwa na polisi hii leo Machi 20, 2023 jijini Nairobi nchini Kenya.

Kabla ya kukamatwa, Waandamanaji hao pia walipambana kwa kuwarushia mawe polisi wa kupambana na ghasia nje ya ofisi za Serikali katika mji huo mkuu, na walijibiwa kwa kurushiwa mabomu ya machozi ambayo yaliwatawanya.

Waandamanani wakikimbia ghasia nchini Kenya. Picha ya AP.

Baadhi ya waandamanaji akiwemo Markings Nyamweya wakiwa wamechoma matairi katika kitongoji duni cha Kibera, walisema, “Tutakuwa hapa hadi gesi ya kutoa machozi imalizike, tunataka unafuu hali ni ngumu na ujumbne huu umfikie Rais (Ruto).”

Odinga, ambaye alishindwa katika uchaguzi wa mwaka jana dhidi ya Ruto, aliwaambia wafuasi wake kushiriki maandamano hayo kupinga upandaji wa bei ya mahitaji ya kimsingi, kushuka kwathamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani na ukame ulioweka rekodi ya kuwaacha mamilioni ya watu njaa.

Rais Samia azindua Programu Kilimo mashamba makubwa
Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi