Aliyekuwa kiongozi wa kundi hatari zaidi la kigaidi la ‘Al Qaeda’, Osama Bin Laden aliacha wosia wa urithi aliouandika kwa mkono wake, uliotaja kiasi cha fedha alichokiacha kwa ajili ya kusaidia vita ya ‘Jihad’ duniani.

Wosia huo umebainika kuwa kati ya nyaraka muhimu zilizotolewa na Serikali ya Marekani, ilizozipata katika jumba alilokuwa amejificha baada ya kikosi maalum cha jeshi la nchi hiyo kumsaka na kumuua mjini Abbotabad nchini Pakistan mwaka 2011.

Jumanne wiki hii, nyaraka hizo ziliwasilishwa kwa vyombo vya habari kwa ajili ya kuueleza umma. Osama alitaja kiasi cha $29 milioni ambacho alidai kipo nchini Sudan, akiitaka familia yake yote kuhakikisha inatii wosia wake huo.

Osama aliyekuwa anatajwa kuwa mtu anayetafutwa zaidi na Marekani Duniani, alionekana kukinusa kifo chake na kumtaka baba yake kuhakikisha anamtunza mkewe na watoto wake baada ya kifo chake.

“If I am to be killed, pray for me a lot and give continuous charities in my name, as I will be in great need for support to reach the permanent home,” aliandika.

Hata hivyo, Osama ambaye alikaa Sudan kwa miaka mitano miaka ya 1990 akifanya kazi kama mhandisi na kusaidia wananchi katika miradi mingi ya barabara na kuchimba visima, hakubainisha kama utajiri wake huo uko katika vitu au ni fedha pekee.

Katika nyaraka nyingine, Osama alionekana kuelezea mtazamo wake kwa vita vya Afghanistan dhidi ya makundi ya Magaidi na Marekani, akiwataka wawe wavumilivu kwani katika uvumilivu kuna ushindi.

“Walifikiri vita itakuwa rahisi na kwamba wangekamilisha malengo yao ndani ya siku chache au hata wiki chache. Tunatakiwa kuwa wavumilivu zaidi. Kukiwa na uvumilivu, kuna ushindi!” aliandika Osama.

Baada ya kuuawa kwa Osama, hivi sasa kundi la Al-Qaeda linaongozwa na Ayman Al-Zawahir.

 

Magufuli atangaza rasmi Sudan Kusini Kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki
SAMATTA AZIDI KUPAA, ATINGA 'GAME YA FIFA'