Wakati Watanzania wakisherehekea na kujivunia mchezaji ‘kipenzi chao’ Mbwana Ally Samatta kufunga bao la kwanza tangu aanze kucheza Ukawa,  imeibuka habari nyingine njema nkuhusu mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji.

Mchezaji huyo amejumuishwa kwenye kikosi cha Genk katika game ya plays tation ya FIFA 16. 

Tayari mashabiki wa soka wameanza kumchezesha mchezaji huyo akiwa na kikosi cha Genk na jezi yake namba77.

Samatta alijiunga na Genk kwa kitita cha Euro 800,000 akitokea kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na Mazembe pamoja na kuwa mfungaji wa michuano hiyo.  Kadhalika, akiwa ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika ya CAF.

Tangu Samatta atue Gene amekuwa akicheza kila mechi. Japokuwa

anatokea benchi, tayari ameshapachika bao la kwanza katika mchezo wake wa tatu tu.

Samatta alifungua akaunti yake mabao katika klabu yake mpya, KRC Genk katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji Jumapili jioni wakishinda 3-2 dhidi ya Club Bruge Uwanja wa Cristal Arena, Genk.

Samatta aliyejiunga na Genk mwezi Januari akitokea TP Mazembe ya DRC, alifunga bao hilo dakika ya 81 akimalizia pasi ya kiungo Ruslan Malinovskiy, baada ya kuingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Nikolaus Karelis dakika ya 79.

Mabao mengine ya Genk siku hiyo yalifungwa na Karelis kwa penalti

dakika ya 36 na Thomas Buffel dakika ya 50, wakati ya Bruge yamefungwa

na Thomas Meunier dakika ya 15 na Hans Vanaken dakika ya 83.

Na ushindi huo, unaifanya Genk ifikishe pointi 45 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kukamata nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji. 

Mabilioni aliyoacha Osama Bin Laden kusaidia ‘Jihad’ yawekwa wazi, aliona kifo chake
‘Paul Makonda Amewatonesha walimu vidonda’