Mwenyekiti wa kikao cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika leo jijini Arusha, Dk. John Magufuli ametangaza rasmi kuwa Sudan Kusini imekubaliwa kujiunga na Jumuiya hiyo, baada ya kupitishwa na viongozi wa nchi hizo.

Hivyo, Jumuiya hiyo sasa inaundwa na nchi sita ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

Kikao hicho kiliikaribisha rasmi Sudan Kusini katika Jumuiya hiyo pamoja na kujadili masuala ya kiusalama wa Kanda nzima ikiwa ni pamoja na hali ya machafuko nchini Burundi.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza hakuhudhuria kikao hicho, lakini alimtuma Makamo wake wa pili, Joseph Butore kumuwakilisha.

Mama yake Halima Mdee alia na serikali ya Magufuli
Mabilioni aliyoacha Osama Bin Laden kusaidia ‘Jihad’ yawekwa wazi, aliona kifo chake