Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, amemtaka waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuwachukulia hatua waliokwamisha mradi wa maji wilayani Masasi mkoani Mtwara kabla hajamchukulia yeye hatua.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo, alipokuwa anaendelea na ziara yake mkoani humo, ambapo amesikiliza kero za wananchi katika vijiji mbalimbali na kuwatatulia kwa maagizo ya papo kwa papo.

Awali wananchi walipo ulizwa kero zao katika eneo hilo la Masasi hawakusita kutaja kero ya maji na umeme, ndipo Rais alipo mtaka Waziri kutolea ufafanuzi na akamtaja mkandarasi kuwa anahusika.

TMA yatangaza mvua kubwa siku mbili

Mkandarasi huyo alipoitwa alisema kuwa wamepewa muda wa miezi sita ili kufanya upembuzi yakinifu katika kukamilisha mradi huo.

“Mkataba mmeuandaa ninyi, kwanini muandae kwa miezi sita?, Waziri nakupa wiki mbili nendeni mkaufute, hamuwezi kufanya upembenuzi yakinifu miezi sita…ni shida kweli mnataka nizungumze mara ngapi nataka wiki mbili wamalize na waanze kujenga”

Kijana avaa kitumwa kuhamasisha uandikishwaji Dar

” Wanadanganya nini hawa…Profesa Mbarawa nenda kalisamamie kama kuna mkataba nenda mkaufute leo nataka maji yapatikane hapa Waziri nimesha kueleza haya sikutakiwa kuzungumza hapa hadharani inaudhi” Amesema Rais Magufuli.

Na kusisitiza kuwa ” Utafukuzwa wewe…ninataka mambo yaende sawasawa fukuza hawa watu kabla hujafukuzwa wewe, hakuna haja ya kuchukua nje mainjinia kama mnao serikalini muwalete hapa mjenge wenyewe”

Kamati za Bunge kujadili taarifa ya CAG

Nimeteuliwa na Rais msataafu ( Benjamin Mkapa)miaka 10 kuwa Waziri kipindi chake chote, Aliye nifundisha kazi Mama Anna Abdallah anatoka hapa Masasi leo hii mnaleta mambo ya ajabu hapa” Amesisitiza Rais Magufuli

Basi la kanisa lanaswa na misokoto 230 ya bangi
Kijana avaa kitumwa kuhamasisha uandikishwaji Dar