Mgombea urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli ameahidi kumshughulikia mtu mmoja aliyemtaja kama ‘kigogo’ wa eneo la Temeke aliyefungua kesi mahakamani kupinga mradi wa maji uliopita katika nyumba yake.

Akiongea katika mkutano wa kampeni, Magufuli alieleza kuwa anatambua kero wanayoipata wananchi wa eneo hilo baada ya ‘kigogo’ huyo kufunga mfereji wa maji na kujenga bomba la maji taka, hali iliyosababisha magonjwa mengi ya mlipuko kama kipindupindu.

Alisema atahakikisha analishughulikia tatizo hilo haraka baada ya kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 “Ninachojua hapa Temeke kuna mtu alikimbilia mahakamani na kuwamisha mradi wa maji lakini mahakama haitoi haki kwa wakati. Zimebaki siku nne mnichague kuwa rais, mtu anachelewesha mradi wa maji kwa kwenda mahakamani! Ngoja nipate urai,” alisema.

“Amejenga juu ya njia ya maji watu wanakufa kwa kipindupindu haki ya Mungu ngoja nipate urais,” aliongeza.

 

 

Waweka Magari na Nyumba Rehani Kutabiri Rais Ajaye , Ni Rukhsa Kushiriki
Video: Lowassa Ajibu Kuhusu Afya Yake, Atakachofanya Endapo Atashindwa, Elimu Bure Na Mengine