Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Februari 13, 2023 ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Songwe ambapo akiwa katika kijiji cha Kaloleni kata ya Mkwajuni ameweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Songwe.

Ujenzi wa hospitali hiyo, ambao umegharimu shilingi bilioni 3.5 mpaka sasa imefikia asilimia 95 ya ujenzi wake ambapo Halmashauri inatarajia kukamilisha Mradi huu tarehe 31 machi 2023, ikiwa ni sambamba na kuanza kutumika rasmi kwa majengo yote ambayo tayari vifaa vyake vimepokelewa.

Hospitali ya Wilaya ya Songwe.

Ujenzi katika hospitali hiyo inahusisha Ujenzi wa Majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, Mionzi, Maabara, ufuaji, Famasia, Utawala na Jengo la Mama na Mtoto, Ujenzi wa Wodi tatu za Magonjwa Mchanganyiko.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi.

Majengo mengine ni jengo la Huduma ya dharula na Nyumba ya Watumishi Familia tatu, jengo la Upasuaji, jengo la Uchunguzi na kuhifadhia maiti na wodi mbili za Upasuaji (Wanaume na Wanawake).

Tanzania kunufaika na Bil 120 miradi uhifadhi wa Mazingira
Mstaafu atishia kujinyonga kwa kulipwa milioni 45