Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, mahandisi Isack Kamwelwe amezindua mfumo wa majaribio wa ukatishaji tiketi wa mabasi kwa njia ya mtandao huku akieleza kuwa njia hiyo italeta tija kwa Serikali, abiria na wamiliki wa mabasi.

Amebainisha kuwa mfumo huo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya mtandao, utaondoa upotevu wa mapato kwa wasafirishaji ambayo maranyingi hupotelea katika mikono ya wapigadebe.

Mhandisi Kamwelwe amesema kwa upande wa abiria matumizi ya mtandao katika ukatishaji tiketi utawaondolea mlolongo wa kufunga safari kwenda vituo vya mabasi siku moja kabla ya safari kwaajili ya kukata tiketi.

“pia utaondoa kero za abiria kubugudhiwa kwenye vituo vya mabasi na kufanya usafiri huu kuwa wa heshima, utakomesha vitendo vya upandaji holela wa nauli hasa kipindi cha mwisho wa mwaka” amesema waziri Kamwelwe.

Aidha amesema kwa upande wa Serikali mfumo huo utawezesha kupatikana kwa taarifa muhimu zenye kusaidia serikali katika maamuzi sahihi kwakuwa ndio kitovu cha usafirishaji nchini.

Amesema mfumo huo utatumika kwa majaribio hadi kufikia juni mwaka huu na baada ya hapo LATRA isitoe leseni kwa mmiliki ambaye hajajiunga na mfumo huo ili kuhakikisha kila mmiliki anatumia.

Jeshi la Ethiopia lakiri kudungua ndege ya Kenya, bahati mbaya
Waliotapeli facebook kwa jina la Mama Magufuli, watiwa Mbaroni