Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ameahidi kulisafisha jiji hilo kwa utendaji wake, ameanza ziara ya kuchota baraka na busara za wazee na viongozi wakuu wa dini mbalimbali.

Jana, Makonda alimtembelea Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mwadhama Kardinali Polycarp  Pengo ambaye pia ndiye Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, ambapo alizungumza naye na baadae kiongozi huyo alimuwekea mikono na kumuombea baraka kwa Mwenyezi Mungu.

Paul Makonda na Kadinari Pengo

Baada ya ziara hiyo, Makonda alisema kuwa amepanga kuwatembelea wazee na viongozi wa dini Mkoani humo kwa lengo la kupata busara zao ili zimsaidie katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Mkoa huu una wazee. Ili uweze kuongoza vyema ni lazima upate busara zao zikusaidie katika majukumu yako,” alisema.

Leo, Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam anatarajia kumtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubery na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

Serikali ya Magufuli Kuwapima watoto 'DNA' kujua wazazi wao halisi
Video Mpya: Vanessa Mdee - Niroge