Mkuu wa Idara Ya Habari Na Mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Ramadhan Manara amewashukia baadhi ya mashabiki ambao wameshindwa kuelewa dhana ya UTANI WA JADI na kuigeuza kuwa ugomvi.

Manara amechukua maamuzi hayo kufuatia vitendo vilivyoibuka siku za karibuni vya baadhi ya mashabiki wa klabu moja kuwapiga wengine, huku wengine wakirushiana matusi ya nguoni kupitia mitandao ya kijamii.

Katika kurasa za mitandao ya kijamii za Haji Manara ameandika:

Kuitana mikia, Utopolo, Gongowazi, Wamatopeni mfano wake haukuanza leo, nikiwa mdogo nilikuwa nasikia kandamili, Biju na hata Abijo,,niliwahi kuona hadi zile za kina dada zinatupwa uwanjani ktk derby moja hv!!

Bad luck zama zile hatukuwa na mitandao Kama hii!!

Na nakumbuka tuliwahi kuambiwa Simba inashindia mihogo na ndege kupanda ni mwiko, kuna wakati tulitaniwa eti twende Coco Beach kufanya Mazoezi kisha tulipwe bila kucheza mechi.

Sitasahau kejeli za watani walipomsajili Mbuyu Twite na Yondan..

Kwa tunaolewa misingi ya uanzishwaji wa hv vilabu wala halina tabu hilo, ndio raha zenyewe za Simba na Yanga.

Tabu inakuja kwa wageni ktk football,,watu ambao klabu hz wamekutana nazo Instagram na Facebook, wakati mwingine hadi baadhi ya Wachambuzi uchwara nao wameingia ktk huu mtego, kiukweli mm siwalaumu coz naamini wanatakiwa wajifunze ,uchanga wao na ufahamu wao ktk hv vilabu ni mdogo mno na hata football yenyew ni mitandao tu inawasaidia, dana dana tatu kupiga mtihani!!

Ukiangalia hyo picha hapo unahisi kabisa lazma kulikuwa na vijembe na kejeli za Usimba na Uyanga,,hyo ndio raha ya football made in Tanzania na niwaambie mm ni MUUMINI mkubwa wa hilo coz najua faida yake kijamii ,,ila hatupaswi kutukanana na kuambiana lugha za kishenzi na ndio maana ni mm niliyetoka hadharani kuwasihi Wanasimba wenzangu wasiwatanie Yanga nyani na Alhamdulillah wengi wao walinisikia,,Kwa sasa tushikilie lile jina letu,,UTOPOLO au tulinakshi kdogo UTO.

Magufuli :Hakuna kulipa ushuru
Kumbe Ntibazonkiza, amecheza Ulaya!