Bondia bingwa, raia wa Ufilipino, Manny Pacquiao amewaomba radhi wote aliowakwanza baada ya kuponda ndoa za jinsia moja na kudai kuwa watu wanaoshiriki ndoa hizo ni  sawa na ‘wanyama’.

Bondia huyo ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge nchini humo, amekuwa akionesha imani thabiti ya Kikristo yeye pamoja na familia yake na mara kadhaa ameonekana akihubiri kanisani.

Kupitia Instagram, Pacquiao amewamba radhi lakini ameendelea kushikilia msimamo wako kutokana na mafundisho ya Kitabu Kitakatifu cha Mungu kuwa ndoa za jinsia moja ni dhambi.

“I’m sorry for hurting people by comparing homosexuals to animals. Please forgive me for those I’ve hurt. I still stand on my belief that I’m against same sex marriage because of what the Bible says, but I’m not condemning LGBT. I love you all with the love of the Lord. God Bless you all and I’m praying for you,” ameandika.

 

 

Mfungaji Bora Wa Ligi Ya Afrika Kusini Afariki Dunia
Rooney Amkingia Kifua Louis Van Gaal