Klabu ya Olympique Marseille imetangaza kuachana na kiungo kutoka nchini Ufaransa Lassana Diarra kwa kuvunja mkataba wake.

Kiungo huyo ambaye aliwahi kuzitumikia Real Madrid, Chelsea na Arsenal, alijiunga na miamba hiyo ya soka nchini Ufaransa Mwezi Julai mwaka 2015 akiwa mchezaji huru, baada ya kumalizana na klabu ya Lokomotiv Moscow ya Urusi.

Diarra ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter: “Leo (Jana) nimeachana na klabu ya Olympique Marseille baada ya kufanya nayo kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu. Ninawatakia kila la kheri wachezaji na viongozi katika harakati zao za kupambana, Tutakua pamoja siku sio nyingi.”

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, alianza maisha yake ya soka kwenye klabu ya Le Havre ya nchini kwao Ufaransa (2004) kabla ya kutimkia England kujiunga na Chelsea (2005–2007), kisha alikwenda Arsenal (2007–2008) kabla ya kujiunga na Portsmouth (2008–2009).

Baadae alielekea nchini Hispania kujiunga na Real Madrid (2009–2012), kisha alitimkia nchini Urusi kwenye klabu ya Anzhi Makhachkala (2012–2013) na baadae Lokomotiv Moscow (2013–2014).

Thomas Tuchel Amkingia Kifua Aubameyang
GK awakumbusha wasanii kurudi shule