Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa Taifa yatakayofanyika kuanzia Mei 29 hadi Juni 4 mwaka huu katika ukumbi wa Manyara Park, Manzese jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga ameeleza kuwa hadi kufikia juma hili timu zilizothibitisha kushiriki ni Ngome Boxing, Bandcoy Boxing, MMJK Boxing, Mgulani JKT Boxing, Kibiti JKT Boxing na Magereza Boxing ambazo zote zinatoka vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa. Timu nyingine ni Dar es Salaam Boxing, Azam Boxing, Kigamboni Boxing na Kimara Boxing zote za Dar.

Nyingine ni Morogoro Boxing, Kibaha Boxing, Kibaha Boxing, Yombayomba Boxing, Manyara Boxing, Tabora Boxing, Mwanza Boxing na Arusha Boxing.

Mashaga amesema mashindano hayo yatatumika kupata timu ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani nchini Ufaransa.

Sambamba na mashindano hayo pia shirikisho hilo litaendesha kozi za makocha na waamuzi wa mchezo wa ngumi kwa hatua ya awali na taifa kuanzia kesho.

TANAPA yatoa ufafanuzi tukio la vurugu Mto wa Mbu
Mamilioni yatumika kukarabati miundombinu vikosi, makambi