Kiungo wa klabu ya Newcastle Jonjo Shelvey amefungiwa kucheza michezo mitano pamoja na kutozwa faini ya Pauni 100,000, baada ya kubainika alitumia lugha ya kuudhi dhidi ya mchezaji wa timu pinzani.

Chama cha soka nchini England FA, kimebaini utovu huo wa nidhamu uliofanywa na Njonjo Shelvey katika dakika ya 87 wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Wolverhampton Wanderers, uliochezwa Septemba 17.

Taarifa ya FA imeeleza kuwa: “Jonjo Shelvey amefungiwa kucheza michezo mitano pamoja na kutozwa faini ya Pauni 100,000 baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha ya kukera dhidi ya mchezaji wa timu pinzani.

“Mchezaji huyu wa Newcastle United amehukumiwa baada ya FA kujiridhisha alitenda kosa hilo.

“Ni makosa kisheria kutoa lugha ya kuudhi ama chafu dhidi ya mpinzani wako mnapokua uwanjani, tunafahamu Njonjo analijua hilo na ndio maana tumeamua kumuadhibu ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.”

Hata hivyo adhabu hiyo imeelezwa kuwa kubwa kutokana na Njonjo kukanusha kufanya kosa hilo, lakini FA walijiridhisha zaidi ya mara moja kwa kufutilia kwa umakini picha za televisheni na matamshi yaliyotolewa kinywani mwake.

Karamoko Dembele Avaa Jezi Ya England
Azam FC Waanza Kuiwinda Majimaji, Kuifuata Kesho