Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imetangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa nchi hiyo na kumtaja Yoweri Kaguta Museveni kuwa mshindi wa kiti cha urais kwa Awamu ya Tano mfululizo.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, Museveni ameshinda baada ya kupata jumla ya kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.7 ya kura zote halali zilizohesabiwa.

Mpinzani Mkuu wa Museveni, Dk. Kiza Besigye ameshika nafasi ya pili katika uchaguzi huo kwa kupata jumla ya kura 3, 270, 290 sawa na asilimia 35 ya kura zote halali zilizohesabiwa.

Matokeo hayo yamempa nafasi Rais Museveni kuliongoza taifa hilo kwa miaka 35 mfululizo tangu alipoingia madarakani mwaka 1986.

Watani wa Jadi: Mnyama Atafunwa
Watani wa Jadi: Simba wajeruhiwa, Yanga wacheka na nyavu zao