Kocha msaidizi wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana Maxwell Konadu, ameteuliwa kuliongoza benchi la ufundi la timu hiyo kwa muda, baada ya Avram Grant kumaliza mkataba wake.

Konadu, mwenye umri wa miaka 44, amekua msaidizi wa kocha mkuu wa kikosi cha Ghana tangu mwaka 2014 baada ya kuondoka kwa Kwesi Appiah, pia aliwahi kuwa kocha msaidizi timu za vijana za Ghana chini ya umri wa miaka 20 na 23.

Uongozi wa chama cha soka nchini humo GFA ulifanya maamuzi ya kumteua Konadu, katika kikao kilichoketi siku ya jumanne na umeafiki kumteua Joseph Mintah kuwa msaidizi wa muda.

Hata hivyo Mintah ametakiwa kufanya kazi ya usaidizi wa ukufunzi, huku akiendelea na shughuli za kutengeneza saikolojia za wachezaji.

Alikiba atoa sababu ya Rapa M.I kutoonekana kwenye video ya Aje Remix
Mbowe na Mkewe wabanwa tena, TRA yawaburuza Mahakamani