Kocha mkuu wa Simba, Jackson Mayanja ameelezea sababu za kumuacha nje ya kikosi cha kwanza kiungo Said Ndemla.

Ndemla amejikuta akitupwa benchi tangu kocha Mayanja aanze kuifundisha Simba. Kiungo huyo wa timu ya Taifa alikuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa wakipewa nafasi kubwa mwanzoni mwa msimu kinyume na sasa.

Kocha Mayanja hakusita kutoa ufafanuzi suala linalopekea Ndemla kupata nafasi ndogo ya kucheza katika kikosi chake.

” Ndemla ni mchezaji mchanga, bado namuandaa kuja kuitumikia Simba kwa siku za usoni. Ni mchezaji mzuri lakini bado hajaiva”

” Pia najaribu kuhakikisha wachezaji wanapokezana, ndio maana unaona hata yeye anapata nafasi kipindi cha pili kama leo.”

Kuhusu Ndemla kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ambaye kwa kutocheza anaiweka rehani nafasi yake ya katika kikosi cha Taifa Stars, Mayanja amejibu kwamba, ”Ndemla

Mimi ni kocha wa timu ya Simba, sipangi kikosi changu kwa rekodi za timu ya taifa au historia ya mchezaji. Nachagua mchezaji aliye fiti kuisaidia Simba”

Serikali yaweka sawa, CT-Scan ya Muhimbili ilihamishwa kutoka UDOM
Guss Hiddink Amedhihirisha Anachokifanya Chelsea