Serikali imeweka sawa taarifa zake kuhusu ununuzi wa mashine ya CT – Scan iliyowekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mwishoni mwa mwaka jana kuwa ilihamishwa kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Khamisi Kigwangalla aliwaambia wabunge kuwa serikali iliamua kuhamisha mashine hiyo kutokana na uhitaji mkubwa uliokuwapo wakati ule katika hospitali hiyo ya Taifa.

“Kilikuwa kipindi kigumu na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inayohudumia wagonjwa kutoka pande zote za nchi, ilihitaji mashine mpya. Hakukua na njia nyingine bali kuhamisha mashine ya Chuo kikuu cha Dodoma kwenda Muhimbili,” alisema Kigwangalla.

“Kitu kizuri ni kwamba Mashine ya Muhimbili itakapowasili, itapelekwa Chuo Kikuu cha Dodoma,” aliongeza.

Naibu Waziri huyo alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) kuitaka Serikali kueleza kama mashine hiyo ilinunuliwa ama ilihamishwa kutoka katika Chuo Kikuu Cha Muhimbili.

 

Azam FC Yatua Dar es salaam, Yaingia Kambini Moja Kwa Moja
Mayanja Awajibu Wanaomtaka Said Demla Kikosini