Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Kagera Sugar Hamis Mazanzala amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo wa Kiporo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa baadae leo Jumatano (Januari 26), kwenye Uwanja wa wa Kitaba mjini Bukoba.

Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Simba SC, katika mchezo huo ambao ulistahili kuchezwa Desemba 12, lakini uliahirishwa na Bodi ya Ligi kutokana na wachezaji wengi wa Simba SC kukutwa na maambukizo ya ugonjwa wa mafua, kukohoa, kichwa na homa kali, hivyo kusababishwa mechi isifanyike kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Akizungumza na Dar 24 Media #taarifabilamipaka, Mazanzala amesema wamejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huo, na wanaamini mambo huenda yakawa mazuri kwa upande wao.

Amesema siku zote Uongozi wa Kagera Sugar unaamini timu yao ina uwezo wa kucheza na yoyote katika Ligi Kuu, lakini kwenye ushindani hutoa nafasi ya heshima kwa mpinzani wao kama ilivyo Simba SC.

“Tunaamini soka lina matokeo matatu, kwa hiyo kwetu sisi kama Kagera Sugar tunajipa nafasi ya kushinda, japo katika soka lolote linaweza kutokea.”

“Unajua katika soka yoyote aliyejiandaa vizuri ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, hivyo pamoja na kujipa nafasi sisi ya kushinda hata Simba SC nao wana nafasi kama hiyo kutokana na maandalizi yao.” Amesema Mazanzala

Simba SC iliyochezwa michezo 12 ya Ligi Kuu msimu huu inashuka Dimbani ikiwa na alama 25 zinazowapa nafasi ya kuwa wapili kwenye msimamo wa Ligi hiyo, huku wenyeji wao Kagera Sugar ambao pia wamecheza michezo 12 wakiwa na alama 13 zinazowaweka kwenye nafasi ya 11.

Kagera Sugar: Hatupendi kinachoendelea Instagram
Ahmed Ally: Tutaonesha soka letu Kaitaba