Uongozi wa Kagera Sugar umesema unapambana ili kufanikisha kuwa na ukurasa rasmi wa Instagram unaotambuliwa kisheria, ili kuondoa picha mbaya inayoendelea kwa baadhi ya wadau wa soka kwa jina lao kutumika vibaya.

Kagera Sugar imekua ni sehemu ya klabu za Ligi Kuu ambazo zinapata wakati mgumu wa kuwa na akaunti zaidi ya moja kwenye kurasa za mitandao ya kijamii, hali ambayo inawachanganya wadau wengi wa soka la Bongo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya klabu hiyo Hamis Mazanzala amezungumza na Dar24 Media #Taarifabilamipaka na kusema: “Tumekua tunahangaikia kupata Tiki ya Bluu (Blue Tick) ili tuweze kutambulika kisheria na mtandao wa Instagram, hii ni kutokana na watu wengi kuitumia klabu hii vibaya kwa kuandika mambo ya kejeli kwenye mitandao ya kijamii.”

“Hali hii sio nzuri kwa klabu kama Kagera Sugar, tutaendelea kupambana ili kupata hadhi ya kuwa na haki ya kumiliki ukurasa wetu wa Instagram ambao utatambulisha rasmi sisi kama klabu.”

Makamu wa Rais awapa maagizo mabalozi
Mazanzala: Tuna nafasi ya kushinda leo