Chama cha ngumi za kulipwa nchini PST kimesema Jeshi la Polisi linaandaa utaratibu ili kuweza kumtia mikononi bondia Thomas Mashali.

Katibu mkuu wa PST Antony Rutta alisema Januari pili mwaka huu, Mashali aliingia katika ukumbi wa Friends Corner akiwa kama mtazamaji wa mapambano maalum ya kufungua mwaka lakini ghafla akaanza kufanya fujo na kurusha chupa zilizokatwa kwa watu mbalimbali ukumbini hapo.

Alisema mazingira yalikuwa yakionyesha kwamba Mashali alikuwa kalewa.

“Aliingia akiwa kalewa sana na kuanza kufanya fujo, moja ya chupa alizorusha ilimpata mmoja wa mabondia waliokuwa ulingoni akipigana”

“Halafu kama hiyo haitoshi akawa anatuma meseji za hovyo kwa viongozi wa PST na watu wengine, kitu ambacho kilinishangaza sana,”alisema.

Alisema baada ya tukio hilo walilazimika kuripoti polisi na sasa wanasubiri hatua zao za kisheria.

Alipotafutwa kwa njia ya simu, Mashali  alipokea na kisha kukata haraka mara baada ya kutambulishwa jina.

Baada ya kukata simu akatuma ujumbe mfupi ulioeleza kwamba yuko hospitali anaumwa sana na hawezi kuongea.

Ubishi Kumalizwa Kisiwani Unguja, Ni Dhambi Mtoto Kutumwa Sokoni
Mwanamama Aliyeinyima Bao Mtibwa Aswekwa Lupango