Mwamuzi aliyekataa bao la pili la Mtibwa Sugar katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC, ameadhibiwa kwa kuondolewa mashindanoni.

Mwamuzi huyo wa pembeni mwanamama Dalila Jafari, usiku wa Jumapili alikataa bao la pili la Mtibwa lililofungwa na Kichuya kwa kichwa akimalizia krosi ya Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kwa kunyoosha kibendera akiashiria kwamba bao hilo lilikuwa la kuotea.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama Cha Soka Zanzibar ZFA, Masoud Attai alisema kamati ya mashindano ilipitia video ya mchezo huo na kujiridhisha kwamba Dalila alikosea.

Alisema lile lilikuwa ni bao halali na pengine Mtibwa ingepata ushindi wa 2-1 badala ya sare ya 1-1.

Alisema mwamuzi huyo amefungiwa katika mashindano hayo pekee lakini ataendelea kuchezesha mechi za Ligi kuu ya Zanzibar.

Hapo jana msemaji wa Mtibwa Thobias Kifaru alisema wanasubiria maamuzi huku wakiendelea kujifua na mechi zingine.

Mbabe Wa Francis Cheka Asakwa Na Polisi Jijini Dar es salaam
Ni Zamu Ya Mbilinge Mbilinge Ya Kombe La FA England