Waumini wa Dini ya kiislamu Kata ya Kabindi Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera wamewaomba wahisani kuwasaidia ujenzi wa msikiti mpya baada ya msikiti wa zamani kuharibika na kuhatarisha usalama wao wawapo ibaadani.

Ombi Hilo limetolewa na Sheikh Ahmad Bilali ambaye ni Sheikh wa Kata hiyo baada ya kupokea Mifuko 20 ya Saruji iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mhandisi Ezra Chiwelesa aliyoiahidi kwenye Baraza la Idd.

Aidha Shikh Bilali amemshukuru mbunge huyo na kumuombea kwa Mungu amuweszeshe kutekeleza Ahadi yake maana amekuwa tofauti na watangulizi wake waliokuwa wakiahidi na hawatekelezi.



Hata hivyo amewomba wadau wa maendeleo kuiga mfano aliouonyesha Mhandisi Ezra wa kujitolea kujenga nyumba za ibaada maana ukisha wekeza kwenye nyumba ya kumuabudia Mungu basi wema wako utalipwa hadi siku ya mwisho.

Akiongea baada ya kukabidhi Saruji hiyo katibu wa mbunge Mashaka Maduka ameeleza dhamira ya Mbunge Chiwelesa kuwa ni kuhakikisha analeta maendeleo kwa wananchi wote wa Biharamulo bila kujali dini wala makabila yao, huku Mwenyekiti wa Ccm Biharamulo Robert Malulu akawaomba waumini hao kuendelea kumuombea Dua njema Mbunge wao.

Rais Samia akutana na Naibu Katibu UN
PICHA: Naibu katibu mkuu wa UN atua Dodoma