Mbunge wa Mpendae kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Salim Hassan Turky amesema kuwa alichokifanya katika suala la Ndege iliyomsafirisha Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu ni kuingia dhamana na si kutoa fedha taslimu ya dola 9,000 za Marekani.
Ameyasema hayo hii leo mara baada ya kuenea kwa habari zenye mkanganyiko kuhusu malipo ya usafiri wa ndege hiyo iliyomsafirisha Mbunge wa Singida Mashariki kwenda kwenye matibabu jijini Nairobi Nchini Kenya.
Amesema kuwa nyaraka inayosambaa katika mitandao ya kijamii inayosemekana kutumwa na Mbunge wa Iringa Mjini kupitia tiketi ya Chadema, Peter Msigwa sio tiketi bali ni Invoice.
“Tusifanye tukio la Tundu Lissu kuwa la siasa, mimi binafsi tukio zima la Mbunge mwenzangu limenisikitisha sana pia limenisononesha sana, nikiwa kama kamishna wa bunge lakini pia ni binadamu kuna kuzaliwa na kuna kufa,”amesema Turky
-
Video: Chadema kuchangia damu nchi nzima
-
CUF inahitaji maombi- Kumbilamoto
-
Lissu anena baada kupata fahamu
Hata hivyo, ameongeza kuwa Spika Ndugai alihangaika kutafuta kibali cha ndege iliyokuwepo kiwanja cha dodoma ambayo ndiyo ilikuwa imsafirishe Lissu lakini ilishindikana ndipo yeye alipoamua kuwapigia jamaa wenye ndege yenye kibali cha kuingia Kenya kwa dhamana yake ndipo walipofanikiwa kumsafirisha Lissu.