Vyama vya Siasa visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kutoa rasimu ya mapendekezo ya kutunga sheria mpya inayohusu mabadiliko katika vyama.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Umoja huo, Renatus Muabhi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa hawawezi kuanza kujadili sheria mpya bila kuwa na rasimu.

“Sisi tunamuomba Msajili wa vyama vya siasa atuopatie kwanza rasimi kabla hatujaanza kujadili sheria, kwani kuanza kujadili sheria bila rasimu ni sawa na kazi bure, vile vile tunamuomba aongeze muda kwani aliotoa ni mfupi,”amesema

Bunge latoa ufafanuzi kuhusu kauli ya Spika Ndugai
Mbunge wa CCM aliyemkodia ndege Lissu atoboa siri