Kuelekea mechi ya Simba dhidi ya Azam itakayochezwa leo, bodi ya ligi kupitia shirikisho la soka Tanzania (TPLB) imepangua ratiba ya mechi hiyo.

Awali mechi hiyo ilipangwa kuchezwa saa 10 kamili katika Uwanja wa Taifa lakini  imepanguliwa na sasa itachezwa majira ya saa 11 jioni.

Uamuzi wa kubadili muda wa mechi hiyo umekuja ili kuwapa nafasi mashabiki watakokuwa katika majukumu yao ya kila siku kupata muda wa kuitazama mechi hiyo.

Mabadiliko mengine ni juu ya Uwanja ambapo awali ilipaswa mechi ichezewe katika uwanja wa Uhuru lakini kupitia Waziri mwenye dhamana ya michezo, Harrison Mwakyembe aliruhusu ipigwe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Patrick Aussems aundiwa mkakati kuhama Simba
Video: Wachawi wa Taifa wanazidi kuumbuka, Daktari awashangaa wanaohoji afya ya Rais Magufuli